G5 world

Lets meet and click..

Latest Articles

Msimu Mpya wa maisha Plus 2010

Dear All!
Heri ya sikukuu ya Chismasi na Mwaka mpya, ni matumaini yangu wote muwazima wa afya njema. Msimu mpya wa shindano la Maisha Plus umekwisha shika hatamu, baada ya kumalizika kwa vipindi vya usaili na kila mkoa kujipatia washindi sasa hatua ya mwisho ya shindano hilo imefikia hatua ya kuelekea kijijini.
Lakini kuelekea katika tukio hilo la kihistoria, Disemba 31 saa tano kamili asubuhi kutakuwa na mkutano wa waandishi wa habari na washiriki 42 waliofanikiwa kuingia katika hatua hii kubwa.Mkutano huu utafanyika katika hoteli ya City Style iliyopo Sinza.

Kila mwandishi aliyetumiwa mwaliko huu athibitishe ushiriki wake kabla ya tarehe 30 saa kumi jioni. kwa njia ya barua pepe au simu na aandike namba yake ya simu.

Maisha Plus (Where Life Makes Sense)

Regards
Mratibu Habari
0717 551355

Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Dec. 30, 2009

MPANGO WA G5 KUANZA KUUZA MIZIKI YA KITANZANIA KWENYE INTERTNET

G5 CLICK ONLINE MUSIC STORE - ENTERTAINMENT ON DEMAND
As it was exclusively announced by G5 CLICK on CLOUDS FM during an interview on XXL (Extra Extra Large) with B12 and Fetty, G5 CLICK ENTERTAINMENT COMPANY is Gonne start selling & distributing Bongo music, Movies & Videos, Artwork, Ringtones, E-Books and Tickets through it’s social network website (www.G5click.com).
This service will be available to people all over the world from January 2010 on FACEBOOK, G5 CLICK & MY SPACE, People will be able to buy music and other stuff from this social networks using ATM CARDS that function online – e.g. VISA

IN THE STORE:
BONGO MUSIC – Singles and Albums
E-BOOKS – This are online books that are in PDF format
ARTWORK – Artist wallpapers, photos, covers, logos etc
RING TONES – This will include Mp3, Mono & Polly tones
TICKETS – Event tickets (Parties, shows, Donations)
BONGO MOVIES & MUSIC VIDEOS

IF YOU WOULD LIKE TO BE PART OF THIS PROJECT IN ANY WAY,
PLEASE CONTACT US THROUGH:


Email:
info@g5click.com ; Phone: +255-714-204490 or +255-713-889878
Web: www.G5click.com

THANK YOU ALL FOR SUPPORTING G5 CLICK ENTERTAINMENT
By G5 CLICK ENTERTAINMENT © 2010

Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Dec. 5, 2009

Use G5click.com on your PHONE

SCREEN SHOT OF G5click.com ON IPHONE

To use G5click.com your phone simply go to www.G5click.com/m or m.g5click.com and if your using an Iphone just go direct to www.G5click.com and it will redirect it self to the G5 Iphone version that you see above..

Comments (1) posted by MUSTAPHA SELEMANI Dec. 2, 2009

HEMED ANAJITAYARISHA KUSUKUMA MZIGO KITAA...!!

Hemed ambaye huimba mahadhi ya RnB, anajipanga kuachia albam yake mchizi pia amenicha kuwa hajashirikisha msanii yoyote. Na sababu ya yeye kufanya hivyo ni kwambaa jamaa anataka kuleta utofauti katika muziki huu wa Bongo Flava. Mzigo utakuwa unaitwa "KING WA MELODY'S sooo....!!!!!! acha tuone yaliyomo yamo....??????

Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Nov. 28, 2009

MATONYA NA KALLAGE SASA DUGU MOJA...!!!

Kama unavyo juwa mwanzoni kulikuwa na utata kati ya Kallage na Matonya kuhusu maswala ya kazi kama unavyo juwa Kallage ni mtayarishaji wa video hapa bongo na Matonya ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kwa maana hiyo hawa jamaa kazi zao zinategemeana hapo ndipo utata ulipoanza na ilifikia hatuwa walikuwa wanaishi kma paka na panya. Lakini kwa sasa utata wote kushinei jamaa wameelewana wapo poa sana na katika kuthibitisha hilo kesho tarehe 27 Matonya atafanya video yake ya wimbo wa MARIAM na mchizi Kallage. Lakini kwa mujibu wa Kallage mwenyewe amesema anataka kumalizana na wale wote aliowakwanza mwanzoni akiwamo Lady Jay Dee.

Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Nov. 28, 2009

CPwaa's PRE - LAUNCHING PARTY.

Its my pleasure to inform all BongoFlava, CPWAA's fans and local muisc supporters that i will have an exclusive pre-launching party on 8th Dec 2009 at Movenpic. Shughuli nzima itaanza na wageni waalikwa (V.I.P) kuanzia saa 2 usiku mpaka 5 usiku na baadae kwa kiingilio cha 15,000 TSH kwa yeyote atayependa kuingia. Usiku huo kutakuwa na uzinduzi wa tovuti zangu 2, mavazi,documentary fupi, nyimbo mpya na video zake bila kusahau Album Preview na perfomance moja ya ukweliiiiii!

Na baada ya hapo, ngoma zote za ukweli zitapigwa na maDJ wakali kutoka jijini Dar, na shangwe hilo litaendelea mpaka kuchwele. looking forward to see you there.

Support local talents, support our music! na tutafika tu.

Cpwaa and Splif star of Flipmode squad having a good conversation at the Busta Rhymes after party, Level 8 Kempinski hotel.

Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Nov. 25, 2009

Ni Grand Finale ya Maisha Plus


Shindano la Maisha Plus linafikia tamati Jumapili, ambapo mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 10 papo hapo baada kudumu kwa siku 56.

Shindano hilo lililoanza Machi 1,2009 linafikia tamati ikiwa ni sehemu ya kwanza na ya pekee katika historia ya mashindano ya uhalisia( Reality Shows) nchini Tanzania.

Mratibu wa shindano hilo, David Sevuri anasema shindano hilo linamalizika huku malengo yakiwa yamefikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Tulilenga kuwawezesha vijana kujitambua,Kuwapa ujuzi kwa kuwafundisha vitu mbalimbali, Kuendeleza vipaji vyao,kuwapa mtazamo chanya wa maisha watazamaji na washiriki,kubadilishana utamaduni na kuburudisha watazamaji, tunajivunia kusema kuwa tumeweza kufanikisha yote haya” alisema.

Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Apr. 22, 2009

‘Eviction’ ya aina yake kufanyika Jumapili

Shindano limebakiwa na washiriki 10 ambao mmoja kati yao ndiye atakayechukua zawadi hiyo kubwa hapo kesho.

Mtoano utaanza kuonyeshwa kupitia TBC1 Jumapili saa tatu asubuhi ambapo kwa kuanza saa nne kamili asubuhi washiriki wawili wataaga na baadae washiriki wengine wataaga saa saba kamili mchana.

Mtoano wa mwisho utafanyika saa mbili na nusu usiku ambapo shindano litakuwa limebakiwa na washiriki watatu tu.


Comments (1) posted by MUSTAPHA SELEMANI Apr. 22, 2009

Mpigie kura mshiriki umtakaye ashinde

Miloni kumi imetengengwa kwa mshindi lakini uamuzi wa kumpa mshindi upo kwa mashabiki ambao ndio waamuzi katika shindano hili.

Maulid 33, Hamis 15, Moshy 19, Abdul 32, Charles 11
Steve 14, Upendo 18, Boniface 20, Teddy 36 Modesta 37


Unaweza kupiga kura kwenye mtandao ambao ni maishaplus.g5click.com au kwa njia ya simu kwenda 15522.

Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Apr. 22, 2009

Maisha Plus kurudi tena

Ni miezi miwili imepita tangu shindano hilo lianze, kutokana na uhalisia wa shindano hilo kureflect maisha ya Watanzania wengi wameomba liendelee kuwepo,kwa mujibu wa waandaaji shindano hilo litarejea baada ya mapumziko ya muda mfupi.

Mraribu wa shindano hilo David Sevuri ameliambia Starehe kuwa kutokana na maoni ya watu wengi shindano hilo litakuwa tena TBC1 baada ya timu ya shindano hilo kijipanga upya.

“Tutarudi tena tukiwa tumeliboresha zaidi shindano hili, lakini watazamaji bado watakuwa na vitu vingi vya kutazama kwa wakati wote ambao hatutakuwepo kijijini kwa kuwa tuna vitu vingi havijaonyeshwa” alisema.

Sevuri alisema kipindi cha Maisha Plus cha Jumapili kitaendelea kama kawaida kwa muda wote wakati ‘season’ II ikisubiriwa.

Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Apr. 22, 2009

Maisha Plus ni nini?

Ni shindano la uhalisia ( Reality Show) ambayo halijawahi kufanyika barani Afrika, ni shindalo linalo 'reflect' maisha halisi ya Mtanzania hasa vijana.

Shindano hili lilianza kuonyeshwa kupitia kituo cha TBC1 Machi 1,2009, Mchakato wa kuwatafuta washiriki 18 ulianza Novemba mwaka 2008 katika kanda nane za Tanzania bara na Visiwani.

Lengo la Maisha Plus ni nini?
1. Kuwawezesha vijana kujitambua
2.Kuwapa ujuzi kwa kuwafundisha vitu mbalimbali kupitia semina na mafunzo mbalimbali wanayopewa.
3. Kuendeleza vipaji vyao
4.Kuwapa mtazamo chanya wa maisha watazamaji na washiriki.
5. Kubadilishana utamaduni
6. Kuburudisha watazamaji.


Malengo ya badae ya Maisha Plus

Mwezi wa saba season II ya shindano hili itaanza na safari hii usaili utafanyika katika mikoa yote ya Tanzania.

Season III ya shindano hili itajumuisha nchi zote za Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi n.k.

Waandaaji wa shindano hili ni kampuni ya dmb Inc inayomilikiwa na Masoud Kipanya, Fransis Bonda na David Sevuri.

Kipindi hutengenezwa na kampuni ya True Vision Production.


Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Apr. 19, 2009

Nani kunyakua milioni kumi?

Nani kata ya hawa 10 atanyakua kitita cha shilingi milioni kumi, Jumapili ya tarehe 26 mmoja kati ya washiriki atakwenda nyumbani na kitita cha shilingi milioni 10.

Je ni Boniface, Maulid, Upendo, Steve, Teddy, Charles, Moshy, Hamis (Kingunge), Modesta au Abdul? endelea kufuatilia habari zao katika mtandao wa maishaplus.g5click.com na Tazama TBC1 kila siku.


Comments (3) posted by MUSTAPHA SELEMANI Apr. 14, 2009

Mwanza Juu

Mkoa wa Mwanza ndio mkoa pekee unaowakilishwa na washiriki wote watatu mpaka katika hatua ya fainali huku mikoa mingine kama Tanga ikiwa imepoteza washiriki wake mapema.

Mwanza inawakilishwa na Moshy Mahona, Boniface Michael na Upendo Peneza ambaye ndiye pekee aliyewahi kuingia kiaangoni huku wengine wakiendelea 'kutesa'.

Mikoa ambayo imepoteza washiriki wake wote ni Tanga, Dodoma na Mbeya.

Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Apr. 14, 2009

Asha na Nassib nje

Baada ya 'Fake eviction' wiki hii washiriki wawili kutoka Zanzibar na Mbeya wameliaga shindano hili ambalo limebakiza wiki mbili lifikie tamati.

Nassib alikuwa mshiriki pekee aliyekuwa amebaki ndani yashindano hilo akiwakilisha mkoa wa Mbeya baada ya Kissa kuondoka wiki tatu zilizopita.

Kuondoka kwa Asha kunamfanya Abdul awe mshiriki pekee anayeiwakilisha Tanzania visiwani katika shindano hili.

Comments (0) posted by MUSTAPHA SELEMANI Apr. 14, 2009

More on G5

ADVERTISEMENT

Latest Activity

Vince and Frank Mayo are now friends
2 hours ago
3 hours ago
3 hours ago
5 hours ago

G5 CLICK ENT. COMPANY ©2009 | About Us | Youtube | Official BLOG

Badges  |  Report an Issue  |  Privacy  |  Terms of Service

G5 IP
G5 hit counter