Nilishawahi kuulizwa hili swali nikabaki najikanyaga kanyaga,
sasa naomba niwashirikishe na nyie nisikie maoni yenu. Wote
ni wana hip hop wenye heshima kubwa hapa Bongo kwa kazi
zao nzuri wanazofanya. Sasa naomba uniambie kati ya Joh
Makini na Fid Q nani mkali kushinda mwenzake na ni kwanini.
SABABU HASA NDIZO NINAZOZITAKA. Nani mkali.....???