Mijadala inayoibuliwa bungeni huwa inalenga kutafutia ufumbuzi wa swala lililo leta mjadala husika, bahati mbaya wanapokuwa wanashindanisha hoja zao mtu mwingine anaweza akaona kama wanabishana, kuona kama wanabishana ni mtazamo wa mtu jinsi atakavyokuwa ameuchukulia huo mjadala, lakini kimsingi mijadala huibuliwa ili kutafutia ufumbuzi wa jambo husika na wala si kubishana,kama ingekuwa ni kubishana mbona vijiwe vya kubishana vipo vingisana mtaani na wala havihitaji elimu.